Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miradi ya UNFPA imetuletea nuru katika maisha yetu hapa Zanzibar-Asia Rashid

Miradi ya UNFPA imetuletea nuru katika maisha yetu hapa Zanzibar-Asia Rashid

Pakua

UNFPA ikiadhimisha miaka 25 ya kongamano la idadi ya watu  na maendeleo ICPD25 ambapo lengo ni pamoja na kutokomeza vifo vya mama na mtoto, kuhakikisha mahitaji yote ya uzazi wa mpango yanawafikia wahitaji na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto  kufikia mwaka 2030, imeendelea kutathmini  mafanikio ya miradi mbalimbali ambayo imeshatekelezwa kote duniani ikiwemo Tanzania bara na visiwani.

Katika makala hii Afisa Mawasiliano mkuu wa shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA nchini Tanzania, Warren Bright anazungumza na Asia Rashid, muhudumu wa kujitolea wa afya ya uzazi kwa vijana kwenye kituo cha Raha Leo ambacho kimejengwa kwa msaada wa UNFPA kisiwani Unguja Zanzibar.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/Warren Bright
Audio Duration
3'23"
Photo Credit
UN Environment