Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya mmoja kwa mmoja kusaidia kufanikisha SDGs

Kampeni ya mmoja kwa mmoja kusaidia kufanikisha SDGs

Pakua

Wiki hii viongozi wa Umoja wa Mataifa wamepitisha azimio la kisiasa la huduma ya afya kwa wote ikilenga kuhakikisha kuwa huduma hiyo inapatikana kwa kila mkazi wa dunia hii ifikapo mwaka 2030. Kando mwa azimio hilo kumefanyika vikao vya kando vikileta wadau wa shirika la afya  ulimwenguni, WHO kujadili na kutathmini mwelekeo wa malengo ya afya na ustawi kwa wakazi wa dunia na  miongoni mwa ni Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya kikwete ambaye ni mwanzilishi wa kampeni ya One By One Target 2030 au mmoja mmoja ifikapo mwaka 2030. Priscilla Lecomte wa Umoja wa Mataifa alikutana na Rais mstaafu Kikwete na kupata fursa ya kuzungumza naye.

Soundcloud
Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ Priscilla Lecomte/ Jakaya kikwete
Audio Duration
2'41"
Photo Credit
UN News/Conor Lennon