Mikakati ya kuhakikisha uhakika wa chakula yangaziwa, Uganda

12 Septemba 2019

Lengo la pilli katika Malengo ya Maendeleo Endelevu au SDGs linachagiza kilimo endelevu ili kuhakikisha uhakika wa chakula na lishe ambapo serikali zimekuwa zikichukua hatua mbalimbali  kuhakikisha lengo hilo linatimizwa ambalo ni msingi wa utekelezaji wa amlengo mengine hasa utokomezwaji wa umaskini.

Miongoni mwa mbinu zinazochukuliwa nchini Uganda ni usambazaji wa mbegu bila malipo kwa wanchi mbegu ambazo serikali inaamini kuwa ni bora kuliko zile za asili.

Lakini viiongozi wa kitamaduni wana mtazamo tofauti kuhusu hilo na kupendekeza uelimishaji zaidi wa jamii kuhusu umuhimu wa kilimo na kuweka akiba ya chakula badala ya kuzingatia kuuza kile wanachovuna ili wakidhi mahitaji ya kila siku, mfano kusomesha watoto kwenye shule zilizo ghali.

Ii kufahamu kwa undani, ungana na John Kibego katika mahojiano yake na Mzee Ashraf Nyorano Mugenyi ambaye ni Waziri wa Itifaki na utamaduni katika Ufalme wa Bunyoro.

 (Mahojiano ya Kibego na Mugenyi)

 

Audio Credit:
Brenda Mbaitsa/ John Kibego
Audio Duration:
4'3"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud