Jamii na serikali wanaitikia wito wa huduma za uzazi wa mpango

24 Septemba 2019

Vikao vya ngazi ya juu vya Umoja wa Mataifa vikiendelea kwenye makao makuu ya Umoja huo jijini New York, Marekani, mashirika ya kiraia nayo yanashiriki katika vikao vya kando kuelezea kile ambacho yanafanya mashinani kuchagiza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs huko mashinani. Miongoni mwa mashirika  hayo ni lile la Restless Development nchini Tanzania ambalo kupitia mradi wa Tutimize ahadi linasaka takwimu kuangazia ni jinsi gani serikali inatekeleza ahadi za usawa wa kijinsia na mkakati wa uzazi wa mpango wa mwaka 2020. Abel Koka kutoka Restless Development Iringa nchini Tanzania anawakilishi shirika hilo kwenye vikao hivyo na Assumpta MAssoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza  naye ili afahamu ni vipi wanasaidia wanawake kujikwamua kimaisha kwa kuwawezesha kupata huduma za uzazi wa mpango. Abel anaanza kwa kufafanua..

Audio Credit:
Brenda Mbaitsa/ Assumpta Massoi/ Abel Koka
Audio Duration:
4'11"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud