Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana Kenya wahamasishana kujiunga kwenye kilimo kinachojali mazingira

Vijana Kenya wahamasishana kujiunga kwenye kilimo kinachojali mazingira

Pakua

Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ukiwa unajumuisha pia suala la hatua kwa tabianchi, vijana nao mwaka huu wanashiriki ipasavyo wakifika makao makuu ya  umoja huo jijini New  York, Marekani kuelezea kile ambacho wanafanya mashinani na kuleta mabadiliko chanya. Miongoni mwao ni Victor Mugo kutoka mtandao wa vijana kuhusu kilimo kinachojali mazingira, nchini Kenya ambaye anashirikiana na vijana kusaidia si tu kuhamasisha waingie kwenye kilimo, bali pia wahakikishe kuwa kilimo chao kina tija na kinafanyi iwe wakati wa mvua au wa jua kwa kuzingatia mabadiliko ya tabianchi. Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alipata fursa ya kuzungumza na Victor ambapo ameanza kwa kufafanua kile afanyacho.

Soundcloud
Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ Assumpta Massoi/ Victor Mugo
Audio Duration
4'13"
Photo Credit
FAO/Alessandro Stelzer