Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN Environment na maandalizi kuelekea mkutano wa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

UN Environment na maandalizi kuelekea mkutano wa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi

Pakua

Kuelekea mkutano wa hatua dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika hapa jijini New York, Marekani mnamo Septemba 23 mwaka huu, watu, serikali na mashirika wamekuwa wakifanya maandalizi yatakoyofanikisha mkutano wa Katibu Mkuu wenye lengo ya kuchagiza nchi kuchukua hatua kwa pamoja kukbailiana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi.

Moja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa ambayo yamekuwa yakifanya kazi ikiwemo mashinani kufanikisha mkutano ni lile la mazingira UN Environment ambapo naibu mkurugenzi mtendaji wake, Joyce Msuya katika mahojiano maalum na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ameelezea baadhi ya maandalizi kuelekea mkutano.

Soundcloud
Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ Joyce Msuya/ Stella Vuzo
Audio Duration
3'52"
Photo Credit
UN Environment