Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchimbaji wa dhahabu wachochea ukatili dhidi ya wanawake, Uganda

Uchimbaji wa dhahabu wachochea ukatili dhidi ya wanawake, Uganda

Pakua

Uchimbaji wa madini hufufua ndoto za nchi husika katika kuinua uchumi wake hasa ikiwa uchimbaji huo unafanywa kwa utaratibu unaofaa.

Na usipofuata kanuni na taratibu sahihi uchimbaji wa madini huibua changamoto lukuki kwa jamii za wenyeji hususan makundi yaliyohatarini zaidi ambao ni watoto na wanawake.  Sekta hiyo huambatana na ukatili wa aina mbali mbali ikiwemo dhuluma za matumizi ya fedha za kigeni ziletwazo na wanunuzi wa madini. Kwa mantiki hiyo ni vyema kwa serikali na wadau wote kuwa macho ili kuzuia changamoto hizo. Uganda ni miongoni mwa nchi ambazo zimekuwa zikihaha kuhakikisha uchimbaji wa madini na mafuta unakwenda bara-abara.

Je, Hali ikoje mashariki mwa nchi mabako shughuli za uchimbaji wa dhahabu zimeanza kushika kasi? Kwako John Kibego.

(Makala ya John Kibego)

 

Soundcloud
Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ John Kibego
Audio Duration
3'47"
Photo Credit
GEF