Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

EAGT na harakati za kutunza afya ya vijana

EAGT na harakati za kutunza afya ya vijana

Pakua

Wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kumefanyika mkutano wa ngazi ya  juu wa viongozi sambamba na vikao vya kando kuchagiza afya kwa wote kama jawabu la kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Suala la afya kwa wote linapigiwa sasa chepuo na vijana wenyewe kupitia programu mbalimbal iikiwemo ile ya kuibua vipaji miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki, EAGT inayoendelea hivi sasa kwenye ukanda huo. Muandaaji na mzalishaji wa kipindi hicho, Lee Ndayisaba alikuwepo jijini New York, Marekani na kushiriki baadhi ya vikao hivyo vya huduma ya afya kwa wote na Priscilla Lecomte wa Umoja wa Mataifa alipata fursa ya kuzungumza naye ambapo Lee anaanza kwa kuelezea uhusiano kati ya afya njema na vipaji.

Audio Credit
Brenda Mbaitsa/ Priscilla Lecomte/ Lee Ndayisaba
Audio Duration
3'56"
Photo Credit
© UNICEF/Arjen van de Merwe