Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila damu huna uhai, ndio maana nahamasisha uchangiaji wake Bungoma:Wengamati

Bila damu huna uhai, ndio maana nahamasisha uchangiaji wake Bungoma:Wengamati

Pakua

Damu ni uhai na bila hiyo huna maisha ndio maana nikaamua kulivalia njuga suala la uchangishaji damu jimboni Bungoma. Kauli hiyo ni yake mke wa gavana wa jimbo la Bungoma nchini Kenya kama wanavyomuita mama wa Bungoma, Caroline Wesonga Wangamati.Maelfu ya kinamama duniani na hususan barani afrika hupoteza Maisha wakati wa kujifungua kwa sababu ya kutokwa na damu nyingi kabla na baada ya kujifungua. Akizungumza na Idhaa ya Kiswahili kandoni mwa mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW63 unaoendelea kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani , Bi. Wengamati amemwelezea Flora Nducha katika makala hii nini kilichomsukuma kuchukua hatua hiyo

Audio Duration
4'24"
Photo Credit
UNFPA/Ollivier Girard