Ajira kwa vijana ndio mustakabali wa taifa
Pakua
Ukosefu wa ajira kwa vijana hususan kusini mwa jangwa la Sahara ni kizingiti kikubwa kwa maendeleo
ya mataifa mengi barani Afrika kwasababu kundi hilo ndiyo nguvu kazi ya kila taifa.
Umoja wa Mataifa kupitia lengo nambari 8 la maendeleo endelevu SDGs, linalosema “ajira kwa wote na ukuaji wa uchumi”
unaendelea kuhimiza serikali na asasi za kiraia kuwawezesha vijana kujikwamua na umaskini kupitia miradi mbalimbali.
Serikali ya Uganda inalitekeleza hilo kupitia mikakakti mbalimbali ya kuwasaidia vijana ikiwemo kufadhili miradi yao ya maendeleo katika uakanda wa ziwa Albert.
Mwandishi wetu wa maziwa makuu John Kibego ametembelea eneo hilo na kutandalia makala hii.
Audio Duration
3'41"