Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mdundiko na ukatili vyahitaji vinamnyima haki msichana Kisarawe Tanzania:Jokate

Mdundiko na ukatili vyahitaji vinamnyima haki msichana Kisarawe Tanzania:Jokate

Pakua

Utamaduni ni kitu kizuri kinachoostahili kuenziwa lakini si kila utamaduni unapaswa kuendelezwa kwani tamaduni zingine zinamkandamiza mwanamke na mtoto wa kike kote duniani.

Kauli hiyo imetolewa na Jokate Mwegelo mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani nchini Tanzania. Katika wilaya hiyo bado utamaduni wa kuwacheza ngoma watoto wa kike maarufu kama (mdundiko) pindi wanapovunja ungo au kuwa vigori kuashiria wamepevuka na wako tayari kuolewa na hata kuwa mama, umekita mizizi na huwafanya wasichana wengi kutotimiza ndoto zao, kuzaa mapema na kukabiliwa na ndoa za totoni.

Akizungumza na Stella Vuzo wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa Dar es salaam Tanzania Stela Vuzo Jokate aliyeanzisha kampeni maalumu ya ukombozi wa mwanamke na msichana wilayani humo anaanza kwa kufafanua changamoto ya ngoma.   

 

Soundcloud

 

Audio Credit
Patrick Newman/Stella Vuzo/Jokate Mwegelo
Audio Duration
3'44"
Photo Credit
UN/Eskinder Debebe