Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dini ina mchango mkubwa katika ukombozi wa mwanamke Rwanda:Mchungaji Mwakasungura

Dini ina mchango mkubwa katika ukombozi wa mwanamke Rwanda:Mchungaji Mwakasungura

Pakua

Dini kama ilivyo na uwezo wa kuwaleta watu pamoja vivyo hivyo ina uwezo wa kumkomboa mwanamke sio Rwanda tu bali duniani kote. Kauli hiyo imetolewa na mchungaji Veronica Mwakasungura kutoka Rwanda anayehudhuria kikao cha kimataifa cha kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW63 kinachoendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York nchini Marekani. Mchungani Mwakasungura anasema nchini Rwanda baada ya mauaji ya kimbari dini ilitumiwa na  wanawake kusambaza amani , upatanisho na maridhiano na tangu wakati huo imekuwa msitari wa mbele jkuchagiza jamii katika masuala mbalimbali ikiwemo maendeleo. Katika makala hii Mchungaji Mwakasungura anajadili na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili kuhusu mchango wa dini hiyohiyo kama nyezo ya ukombozi wa mwanamke Rwanda na nini sekta hiyo inafanya kuhakikisha lengo hilo linatimia. Mchungaji Mwakasungura anaanza kwa kueleza fursa waliyonayo.

Audio Credit
Flora Nducha/ Patrick Newman
Audio Duration
4'17"
Photo Credit
UN News Kiswahili/ Grece Kaneiya