Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Najitahidi kuongea na barbaru ili waepuke vishawishi na kutimiza ndoto-Bi. Maina

Najitahidi kuongea na barbaru ili waepuke vishawishi na kutimiza ndoto-Bi. Maina

Pakua

Mimba za utotoni ni moja ya changamoto zinazokabili barubaru katika jamii nyingi duniani ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA linasema kila siku katika nchi zinazoendela wasichana barubaru walio chini ya umri wa miaka 18 hujifungua, hii ikiwa ni sawa na watoto milioni 7.3 wanaozaliwa kila siku. Na iwapo mimba zote zikijumuishwa idadi ya mimba za utotoni itakuwa juu zaidi.

Kwa kulitambua hilo kama changamoto inayokwamisha wasichana wengi kukatisha masomo yao na kutofikia ndoto zao,  nchi na mashirika ikiwemo watu binafsi wamechukua hatua za kukabiliana na changmaoto hizo.Mmoja wa watu ambao wamechukua hatua kama hizo ni Phoebe Maina mwanzilishi wa shirika la Dignified Children International. Katika mahojiano na Grace Kaneiya wa Idhaa ya Kiswahili kandoni mwa mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW63 amemwelezea kuhusu kazi wanazozifanya mashinani huko kaunti ya Nyeri nchini Kenya. Kwanza ananza kwa kuzungumzia yaliyaomkumba kama barubaru na kuchochea kuanzisha shirika hilo.

Audio Credit
Patrick Newman/Grace Kaneiya/Phoebe Maina
Audio Duration
4'33"
Photo Credit
UN /Rick Bajornas