Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pamoja na wanawake na watoto wa Tanzania, pia tunawasaidia wakimbizi-WLAC

Pamoja na wanawake na watoto wa Tanzania, pia tunawasaidia wakimbizi-WLAC

Pakua

Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na  asasi mbalimbali za kiaraia, pamoja na serikali wamekuwa mstari wa mbele kutekeleza ahadi ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030 kupitia malengo 17 yaani SDGs.

Lengo namba 16 la maendeleo endelevu linalenga kukuza utawala wa kisheria katika ngazi ya kitaifa na kimataifa na kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa kila mtu. Kituo cha msaada wa kisheria cha WLAC nchini Tanzania kinautekeleza wito huo kwa kutoa msaada wa kisheria si tu kwa wanawake na watoto bali pia wakimbizi kama anavyoeleza Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho wakili Theodosia Muhulo Nshala katika mazungumzo haya na Flora Nducha wakati wa mkutano wa 63 wa kutathimini hali ya wanawake duniani CSW63 mjini New York Marekani.

Audio Credit
Arnold Kayanda/Flora Nducha/TheodosiaMuhulo Nshala
Audio Duration
8'24"
Photo Credit
UNnewskiswahili/Patrick Newman