Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miundombinu ya kisheria imesaidia kumnasua mwanamke na mtoto wa kike Tanzania- Dkt. Jingu

Miundombinu ya kisheria imesaidia kumnasua mwanamke na mtoto wa kike Tanzania- Dkt. Jingu

Pakua

Mkutano wa 63 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW ukiendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, wajumbe kutoka nchi mbalimbali wanajinasibu na kile ambacho wanafanya kuimarisha usawa wa jinsia na kumsongesha mwanamke na mtoto wa kike. Miongoni mwa wajumbe hao ni wale wa kutoka Tanzania na  hususan Dkt, John Jingu, ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto kuhusu miundombinu ya kisheria ambayo inatumiwa na nchi hiyo kuimarisha usawa wa jinsia. Katika mahojiano na Assumpta Massoi wa Idhaa ya Umoja wa Mataifa anaelezea miundombinu ya kisheria ambayo kwa njia moja au nyingine imeweza kufungua fursa kwa mwanamke na mtoto wa kike wa kitanzania.

 

Soundcloud
Audio Credit
Grace Kaneiya/ Assumpta Massoi/ John Jingu
Audio Duration
4'14"
Photo Credit
Warren Bright/UNFPA Tanzania