Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida 01 Februari 2022

Jarida 01 Februari 2022

Pakua

Miongoni mwa tuliyonayo hii leo kutoka Umoja wa Mataifa 

Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO limetoa ripoti mpya inayoonesha kuwa mifumo ya usimamizi wa taka za afya duniani kote hivi sasa imezidiwa uwezo kutokana na maelfu ya tani za taka zinazotokana na vifaa vilivyotengenezwa kwa ajili ya kukabiliana na janga la coronavirus">COVID-19 na hivyo kutishia afya ya binadamu na mazingira na wakati huo huo kufichua hitaji kubwa la kuboresha udhibiti wa taka zinazozalishwa kutokana na huduma ya tiba. 

Tathmini mpya ya uhakika wa upatikanaji wa chakula iliyotolewa mwishoni mwa mwezi Januari 2022 na Shirika la Umoja wa Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP, inaonesha takriban asilimia 40 ya wakazi wa Tigray Ethiopia wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula ikiwa ni miezi 15 ya migogoro kaskazini mwa Ethiopia. 

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO linasema ingawa teknolojia ya ufugaji wa Samaki nchini Zimbabwe imekua bado lengo la kufanikisha uhakika wa chakula kwa kuhakikisha Samaki anafika mezani bado linakabiliwa na changamoto kwa kuwa gharama ya ufugaji ni ya juu halikadhalika gharama ya kitoweo hicho. 

Na leo mashinani tunakwenda nchini Bangladesh ambako mradi wa ILO umemgeuza mtoro wa shule kuanza kupata kipato ambacho hakutarajia. Karibu! 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
13'3"