Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida 07 Februari 2022

Jarida 07 Februari 2022

Pakua

Miongoni mwa yaliyomo 

ikiwa ni siku moja baada ya ulimwengu kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji wa wanawake na wasichana, FGM, tunaangazia harakati za Umoja wa Mataifa, wadau na wanaharakati katika kufanikisha kuelimisha umma kuhusu ubaya wa matendo hayo. 

Baadhi ya wanawake waliokuwa ngariba nchini Tanzania watangaza kuacha vitendo hivyo vya kikatili katika kongamano liloandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA kwa kushirikiana na Serikali na wadau wa Mtandao wa Kutokomeza Ukeketaji lililofanyika mjini Tarime mkoani Mara. 

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO nchini Tanzania limekabidhi seti 14 za televisheni na kompyuta ndogo 9 kwa serikali ya mkoa wa Kigoma ili kusaidia kusongesha uelewa wa jamii kuhusu masuala ya lishe na kutumia pia mawasiliano ya kidijitali katika kuimarisha sekta ya kilimo. 

Wajumbe wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu nchini Sudan Kusini hii leo wanaanza ziara ya tisa nchini humo. 

Na leo mashinani tunakwenda nchini Kenya katika jamii ya wakuria kusikia mama aliyeamua kuondokana na mila potofu ya ukeketaji na changamoto anazokumbana nazo. Karibu!    

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
9'57"