19 JUNI 2023
Leo jarida la Umoja wa Mataifa linaangazia siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono katika mizozo ya vita, Umoja wa Mataifa umesema jinamizi hilo ni janga lililokita mizizi katika kukosekana kwa usawa, kanuni na tamaduni kali za masuala ya kijinsia.
Utasikia pia kuhusu maonesha ya athari ziletwazo na kauli za chuki ambapo wawakilishi watatu wa taasisi ya Kina mama wa Srebrenica walitembelea maonesho hayo na kuzungumzia maswahibu yaliyowakumba miaka 28 iliyopita na kuacha vidonda katika mioyo yao.