Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

09 JUNI 2023

09 JUNI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia mizozo nchini Sudan ka pia nchi jirani Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Somalai na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?

  1. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binaadamu, OHCHR imeeleza kusikitishwa na athari mbaya za mapigano kwa raia zinazoendelea nchini Sudan ambapo mpaka hizi sasa wamepokea taarifa za kuuawa kwa raia ikiwemo watoto na wajawazito na ubakaji huku waandishi wa habari wakiwa katika hali mbaya kutokana na kauli za chuki hususani mitandaoni.
  2. Na tukitokea huko Sudan tuelekee katika nchi jirani, Sudan Kusini. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini UNMISS umetoa wito wa kusitishwa mara moja kwa uhasama miongoni mwa wakimbizi wa ndani katika Kambi ya Umoja wa Mataifa ya Ulinzi wa Raia nchini humo kufuatia tukio la jana Alhamis ambapo watu kadhaa waliripotiwa kujeruhiwa na wengine kuuawa.
  3. Makala ambayo leo inatupeleka katika majimbo ya Hijraan na Galmudug nchini Somalia yaliyoathirika vibaya na ukame ulioleta changamoto ya maji kwa wakulima na wafugaji, lakini sasa asante kwa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO mradi wake wa maji unaleta nuru.
  4. Na katika tunakupeleka nchini Tanzania kusikia ni kwa jinsi gani mashirika ya Umoja wa Mataifa wanashirikiana na wadau wake kupambana na magonjwa ya kuambukiza.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
9'56"