Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 JUNI 2023

19 JUNI 2023

Pakua

Leo jarida la Umoja wa Mataifa linaangazia siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono katika mizozo ya vita, Umoja wa Mataifa umesema jinamizi hilo ni janga lililokita mizizi katika kukosekana kwa usawa, kanuni na tamaduni kali za masuala ya kijinsia.

Utasikia pia kuhusu maonesha ya athari ziletwazo na kauli za chuki ambapo wawakilishi watatu wa taasisi ya Kina mama wa Srebrenica walitembelea maonesho hayo na kuzungumzia maswahibu yaliyowakumba miaka 28 iliyopita na kuacha vidonda katika mioyo yao.

Makala hii leo inaangazia taarifa za viwavi jeshi kuibuka tena nchini Kenya na juhudi za FAO kukabiliana navyo ikiwemo kuwapatia mafunzo maafisa wa nchi za pembe ya Afrika wanaohusika na kupambana na wadudu hao.

Na mashinani tunaenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia  Kongo DRC ambapo utamsikia afisa wa jeshi la polisi anayehakikisha ulinzi wa wanawake na wasichana wanaokabiliwa na vitendo kwa ukatili wa kijinsia. 

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
14'13"