Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

12 JUNI 2023

12 JUNI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia ajira kwa watoto na wakimbizi nchini Jordan. Makala tunakupeleka nchini CAR na mashinani nchini Kenya, kulikoni?

  1. Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa dhidi ya Ajira au Utumikishaji wa Watoto ambayo inakusudia kutumika kama kichocheo cha kuongeza harakati za kimataifa dhidi ya ajira au utumikishwaji kwa watoto na ikisisitiza uhusiano kati ya haki za kijamii na ajira kwa watoto, kama ilivyo kwa nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa, Tanzania nayo imeungana na mataifa mengine kuadhimisha siku hii ambapo maadhimisho hayo yamefanyika Kitaifa katika kijiji cha Gua.
  2. Katika kambi ya wakimbizi ya Za’atari iliyoko nchini Jordan, roho ya ubunifu ya mtu mmoja na dhamira yake isiyoyumba imebadilisha vitu mbalimbali vinavyotupwa na kuonekana havifai tena kuwa nyenzo muhimu za urembo.
  3. Katika makala leo Afisa Habari wa Kikosi cha 6 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, TANBAT 6 wanaohudumu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, anatupeleka katika ziara ya walinda amani hao kukagua miradi ambayo wameianzisha kwa ajili ya wananchi.
  4. Na mashinani tutakupeleka kijinini Kareman katika kaunti ya Turkana nchini Kenya kushuhudia jinsi ambavyo wenyeji wanajitolea kuhakikisha wanawake na watoto wanaweza kufikia huduma za afya licha ya ukame ambao umezikumba jamii za kaunti hiyo kwa muda mrefu.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, Karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
10'55"