Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

13 JUNI 2023

13 JUNI 2023

Pakua

Hii leo ni Siku ya Kimataifa ya Uelewa Kuhusu Ualbino na kama ilivyo ada ya kila Jumanne tunakuletea mada kwa kina ambapo tutamsikia mwanamuziki Roben X akieleza kuhusu maisha yake ya Ualbino. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za DRC, Myanmar na Ukraine.  Mashinani tunasalia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa tukikuletea ujumbe kuhusu ujumuishaji na uajiri wa watu wenye ualbino.

  1. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limesema imeshtushwa na shambulio dhidi ya kambi ya wakimbizi wa ndani lililofanyika jana Jumatatu  katika jimbo la Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
  2. Nchini Ukraine Umoja wa Mataifa unashirikisha serikali ya taifa hilo na ya Shirikisho la Urusi ili kuhakikisha upatikanaji wa fursa ya kuwafikia raia wote walioathiriwa na uharibifu mkubwa wa bwawa la Kakhovka.
  3. Na mwezi mmoja baada ya kimbunga Mocha kupiga Magharibi mwa Myanmar, mratibu mkazi na wa misaada ya kibinadamu wa umoja wa Mataifa Ramanathan Balakrishnan amesema leo kwamba baraza la uongozi wa jimbo la Rakhine limesitisha fursa ya kufikisha misada ya kibinadamu katika jimbo hilo na hivyo kuathiri usambazaji wa misaada ya kuokoa Maisha katika jamii zilizoathirika.
  4. Na katika mashinani leo nampisha  Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wenye ualbino.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
11'8"