Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

16 JUNI 2023

16 JUNI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia manufaa ya utumaji pesa kutoka nchi moja kwenda nyingine, na uwezeshaji wa wavuvi nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Rwanda na mashinani nchini Colombia, kulikoni?  

  1. Leo ni Siku ya Kimataifa ya Utumaji fedha kwa familia ambapo maadhimisho ya mwaka huu yanaangazia manufaa ambayo ujumuishaji wa kidijitali na kifedha unapohusishwa na utumaji pesa kutoka nchi moja kwenda nyingine, huzisaidia familia zinazopokea fedha kufikia Malengo yao ya Maendeleo Endelevu, SDGs.
  2. Mkuu wa Mpango wa umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS ambaye pia ni mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nicholas Haysom amefanya ziara maalum ya kutembelea visiwa vilivyopo katika kaunti ya Terekeka na kujionea utekelezaji wa miradi ya stadi za maisha inayoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO. 
  3. Makala leo inatupeka mji mkuu wa Rwanda Kigali ambako shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO wiki hii limezindua mradi mpya wa “Kuimarisha huduma za hali ya hewa na tahadhari ya mapema katika Ukanda wa Afrika Mashariki” ukijumuisha nchi zote sita za ukanda huo ambazo ni Kenya, Tanzania, Rwanda, Uganda, Burundi na Sudan Kusini.
  4. Na katika mashinani na tukielekea siku ya wakimbizi Duniani, tutakupelekea nchini Combia kusikia jinsi mwansheria ambaye amelelewa katika kambi ya wakimbizi wa ndani Maisha yake yote na hatimaye kuweza kutimiza ndoto yake ya kuwa mwanasheria ameamua kuzihudumia jamii zilizo chini ya tishio la kigaidi.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'37"