Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

14 JUNI 2023

14 JUNI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia watoto katika migogoro ya silaha na wale wanaokimbia makazi yao.  Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani tunasalia huko huko Tanzania, kulikoni? 

  1. Katika kuelekea siku ya wakimbizi duniani itakayoadhimishwa wiki ijayo, ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imeonya kwamba idadi inayoongezeka ya watoto kutawanywa duniani, inadhihirisha jinsi gani dunia ilivyoshindwa kushughulikia mizizi ya watu kutawanya na kutoa suluhu ya muda mrefu hususan kwa watoto wanaolazimika kukimbia makwao.
  2. Kufuatia vita inayoendelea nchini Sudan, watoto 297 wamehamishwa kwa usalama kutoka kituo cha watoto yatima cha Mygoma huko Khartoum nchini Sudan hadi kituo cha muda katika eneo salama zaidi nchini humo. 
  3. Katika makala taasisi 16 nchini Tanzania zikiwemo mashirikia yasiyo ya kiserikali, asasi za kiraia na vyuo vikuu ambao kwa pamoja ni wanachama wa Mtandao wa Elimu Afrika Mashariki (RELI) wamekutana mjini Morogoro, Tanzania kujengewa uwezo wa namna ya kuimarisha juhudi za kuchochea mabadiliko ya elimu na kuhamasisha ujengaji fikra tunduizi kwa vijana ili kusongesha lengo namba 4 la Malengo ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo Endelevu SDGs.
  4. Na katika mashinani tutaelekea katika shule ya msingi ya Mazimbua-A nchini Tanzania kusikiliza jinsi ambavyo elimu shirikishi inanvyowasaidia wanafunzi sio tu kuelewa kile wanachofundishwa bali pia kujua umuhimu wa kutunza misitu.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
15'24"