Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 JUNI 2023

15 JUNI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo inatupeleka Congo DRC kusikia kinachowasibu wakimbizi wa ndani waliofurishwa na waasi wa ADF na kinachofanywa na Umoja wa Mataifa kuwasaidia. Pia tunakuletea habari kwa ufupi za IOM, UNITAMS na WMO. Katika kujifunza lugha ya tunabisha hodi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA kufafanuliwa maana ya neno "KUYEYESA" 

  1. Tangu mwaka huu uanze mwezi Januari mpaka mwezi huu wa Juni, Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM limerekodi takriban watu milioni 1 walioyahama makazi yao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC kutokana na machafuko yanayotekelezwa na vikundi vya wanangambo.
  2. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusimamia kipindi cha mpito nchini SUDAN, UNITAMS umelaani vikali mauaji ya Gavana wa jimbo la Darfur Magharibi Khamis Abdullah Abbaker yaliyotekelezwa hapo jana na kutaka wale wote waliohusika kufikishwa mbele ya sheria. 
  3. Na tarifa ya kila mwaka ya ‘Kutoa tahadhari mapema kwa kila mtu” iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa WMO imeeleza kuwa juhudi kubwa zilizofanywa na nchi mbalimbali mwaka jana 2022 za kuweka mifumo ya kutoa taarifa za mapema kuhusu majanga ya hali ya hewa zinakadiria kuwa wastani wa watu milioni 111 wapo katika mazingira mazuri ya kujulishwa mapema kuchukua tahadhari.
  4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunafafanuliwa maana ya neno "KUYEYESA" na mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, BAKITA.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'23"