Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 JUNI 2023

08 JUNI 2023

Pakua

Hii leo ni siku mada kwa kina na jaridani tunaangazia siku ya kimataifa ya bahari inayohimiza kuhakikisha bahari inakuwa safi na yenye afya ili iweze kuihudumia vyema jamii tutaangalia namna taka zinazotolewa baharini zinavyoweza kutumika kama malighafi bora ndani ya jamii. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo …. Na katika kujifunza kiswahili tunabisha hodi kwenye Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania BAKITA kufafanuliwa maana ya neno"RUWI", salía hapo hapo!

  1. Katika siku ya bahari duniani ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akisema bahari ni msingi wa maisha na binadamu tunaitegemea bahari lakini je bahari inaweza kututegemea?    
  2. Ethiopia inakabiliwa na dharura nyingi huku kukiwa na changamoto kubwa ya  ufadhili duni limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na kuongeza kuwa huku kukiwa na watu wapya na wanaoendelea kutawanywa  na kuteseka kutokana na ukame, nchi hiyo ya Afrika Mashariki inahaha kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya watu waliokimbia makazi yao nchini kote.
  3. Na tukamilishe na habari Njema. Mlipuko wa homa ya Marburg nchini Equatorial Guinea umemalizika leo kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO huku kukiwa hakuna mgonjwa yeyote mpya aliyeripotiwa katika muda wa siku 42 zilizopita baada ya mgonjwa wa mwisho kuruhusiwa kutoka baada ya matibabu. Mlipuko huo, ambao ulitangazwa tarehe 13 Februari, ulikuwa wa kwanza wa aina yake nchini Equatorial Guinea. Jumla ya wagonjwa 17 walithibitishwa na maabara na vifo 12 vilirekodiwa.
  4. Na katika kujifunza Kiswahili, leo tunafafanuliwa maana ya neno "RUWI" na mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, BAKITA.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, Karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
11'20"