Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

07 JUNI 2023

07 JUNI 2023

Pakua

Jaridani hii leo tunaangazia siku za Umoja wa Mataifa na wawakimbizi wa Sudan wanaolelekea nchi jirani. Makala tunakupeleka nchini CAR na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?

  1. Leo ni siku ya usalama wa chakula duniani, mwaka huu ikibeba kaulimbiu “Viwango vya chakula huokoa maisha” ikilenga kuchagiza mwenendo na viwango vya usalama ambavyo hupunguza hatari ya uchafuzi wa chakula.    
  2. Wakati dunia ikijiandaa kuadhimisha siku ya habari duniani hapo kesho Juni nane shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO limesema ni vyema jamii kuzingatia afya ya baharí kwani umuhimu wake kamwe hauwezi kupuuzwa.
  3. Katika makala Anold Kayanda anatupeleka katika kijiji cha Am Dafock kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linafanya kila namna kuwasaidia wakimbizi waliovuka mpaka wakitokea Sudan.
  4. Na katika mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe wa mshikamano kutoka kwa wanaharakati wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs unaopigia chepuo utokomezaji wa ukatili wa kijinsia.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, Karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'5"