Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

16 Juni 2022

16 Juni 2022

Pakua
Katika Habari kwa Ufupi Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limesema bara la Afrika linaimarisha kasi ya utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 miongoni mwa watu walio hatarini zaidi na dalili zinaonesha mwelekeo ni mzuri. ===== Wafanyakazi wa majumbani licha ya umuhimu wa mchango wao katika jamii wa kutoa huduma ya malezi kwa familia na kaya kwa ujumla, bado wanasalia kutothaminiwa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO. ==== Na kufuatia wito wa wataalamu wa Umoja wa MAtaifa wa haki za binadamu wa kutaka Tanzania isitishe zoezi la kile kinachodaiwa kuwa kumega ardhi ya asili ya wamasai huko Loliondo mkoani Arusha, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi, Balozi Hoyce Temu amesema kumega eneo hilo kumefanyika baada ya mashauriano na kwamba waliodai kushambuliwa hawajajitokeza. Mada yetu kwa kina inamulika mradi wa kunufaisha manusura wa ukatili wa kingono ikiwa ni katika kuelekea siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kingono kwenye maeneo ya mizozo tarehe 19 mwezi huu wa Juni Katika kujifunza kiswahili inafafanuliwa methali, "NJIA PANDA ILIMSHINDA FISI”
Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
13'40"