Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

28 Juni 2022

28 Juni 2022

Pakua

Karibu kusikiliza jarida ambapo wakati mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari ukiendelea mjini Lisbon, Ureno kujadili suluhu za kukabiliana na changamoto za bahari tunakuleta mada kwa kina ikimulika eneo la Vanga Kilifi huko Kenya wanachi wamepata moja ya suluhu kubwa ambayo ni kuvuna na kuuza hewa ukaa kutoka kwenye mikoko kupitia mradi wa Vanga Blue Forest VBF, ambao kwa kiasi fulani unafadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP

Pia utapata fursa ya kusiliza habari kwa ufupi zinazoangazia vifo vya waafrika 23 waliokuwa wanataka kuvuka kwenda Ulaya, tume ya haki za binadamu yaeleza vifo vya watu nchini Kenya ni zaidi ya asilimia 1.5 ya wananchi wa taifa hulo na utasikia kauli ya mmoja ya wanao hudhuria mkutano wa bahari huko Ureno. 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'40"