Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

20 Juni 2022

20 Juni 2022

Pakua

Jarida hii leo linajikita na siku ya wakimbizi ambapo mwenyeji wako Leah Mushi anaanza na ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ya kwamba kusaka hifadhi ni haki ya msingi ya kila binadamu. Kisha anakupeleka Canada jimboni Nova Scotia ambako wakimbizi kutoka kambini Kakuma nchini Kenya siyo tu wamepata hifadhi bali pia wameajiriwa kupitia mpango maalum wa UNHCR, serikali ya CANADA na shirika la kiraia la kupatia ajira wakimbizi kwenye stadi. Makala ni Iran huko ambako mradi wa kupatia bima wakimbizi umeleta ahueni kwa familia ya mkimbizi mwenye mahitaji makubwa kiafya. Mashinani nako ni ujumbe kuhusu wakimbizi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
9'57"