Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

29 Juni 2022

29 Juni 2022

Pakua

Karibu kusikiliza jarida likiletwa kwako na Assumpa Massoi akiangazia

  1. Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO imesema ongezeko kubwa la ufugaji wa samaki sambamba na uvuvi wa kimataifa umesababisha mazao ya vyakula vya majini kuwa kwenye rekodi ya juu katika kuchangia kwa kiasi uhakika wa chakula na lishe katika karne hii ya Ishirini na moja. 
  2. Mvuvi aliyehamia kulima mwani nchini Kenya aeleza anavyopata faida zaidi hivi sasa. 
  3. Makala ikimulika kauli ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhusu kiswahili kutumika kufundishia katika nchi yake.

Na mashinani utamsikia Elvira Alvarado mwanabiolojia wa baharini kutoka taasisi ya Ecomares akieleza harakati za kurejesha matumbawe baharini.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'22"