Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

28 Desemba 2021

28 Desemba 2021

Pakua

Hii leo jarindani tunaanzia nchini Cote D’Ivoire ambako shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeleta matumaini makubwa kwa wakimbizi ambao maisha yao kiuchumi yalitwamishwa na COVID-19. Kisha tunasikia ujumbe wa mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO kuhusu mwelekeo wao wa 2022 na mafanikio yao mwaka 2021 hasa kutokana na kujumuisha vijana katika kufanikisha upatikanaji wa chakula. Tunabisha hodi pia Jamhuri ya Afrika ya Kati ambako walinda amani wa Tanzania #TANBAT5 wanatuma salamu za mwisho wa mwaka na heri ya mwaka mpya huku wakitoa shukrani. Makala ni Kenya kusikia kijana kutoka kabila la wakurya akisongesha harakati za kuepusha watoto wa kike kukeketwa na mashinani sauti kutoka Nigeria ya mwanamke anayepita nyumba kwa nyumba kuhakikisha ugonjwa wa polio unatokomezwa. Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'46"