Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

30 DESEMBA 2021

30 DESEMBA 2021

Pakua

Katika Jarida la habari hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Kenya limechukua hatua ya kushirikiana na viongozi wa dini ikiwemo wale wa madhehebu ya kiislamu ili kusaidia kuelimisha waumini wao juu ya chanjo ya COVID-19 na faida zake katika kuepusha maambukizi

-Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na masuala ya afya ya uzani UNFPA limezindua kampeni ya Hakimiliki ya mwili kwa lengo la kukabiliana na ukatili wa kijinsia mtandaoni hususan dhidi ya wanawake na wasichana 

-Mabadiliko ya tabianchi yamekuwa mwiba kwa wafugaji wa wilayani Ngorongoro mkoani Arucha nchini Tanzania ambapo sasa maji yamekuwa haba na kuathiri mifugo yao

-Makala yetu leo inatupeleka Kenya ambako mwandishi wetu Jason Nyakundi anazungumza na Dorcas Mwachia kijana mwanafunzi wa Chuo Kikuu, ambaye hujitafutia mahitaji ikiwemo karo kwa kutengeneza na kuuza mapambo, baadhi akiyatengeneza  kwa kutumia chupa zilizotumika.

-Na mashinani tuko Sudan Kusini kwa mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS akizungumzia hali ya haki za binadamu na nini kifanyike.

Audio Credit
UN News/Assumpta Massoi
Audio Duration
12'6"