Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

29 Desemba 2021

29 Desemba 2021

Pakua

Hii leo jaridani ni siku ya nada kwa kina tukibisha hodi kwenye makazi ya wakimbizi ya Kyangwali huko Hoima nchini Uganda kusikia tathmini ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuhusu mwaka huu wa 2021 na matarajio yao kwa mwaka 2022. Hata hivyo kuna habari kwa ufupi ikiwa na salamu za mwaka mpya za Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akitaka dunia iazimie kuwa mwaka 2022 ni mwaka wa kujikwamua kutoka kwenye madhila. Na mashinani tunabisha hodi Ufilipino, taifa lililopigwa na kimbunga Rai mwezi huu na sasa wananchi wanaelezea kile walichoshuhudia. Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'10"