Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juni 30 2021

Juni 30 2021

Pakua

Katika Jarida hii leo utasikia huko Paris nchini Ufaransa kumeanza jukwaa la siku tatu la kusaka kusongesha usawa wa kijinsia kwa kujumuisha vijana katika kufanikisha lengo hilo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs ya Umoja wa Mataifa. Mkutano huo unafanyika kwa kuzingatia kuwa miaka 25 baada ya mkutano wa kimataifa wa wanawake huko Beijing nchini China, bado usawa wa jinsia unasalia ndoto kwa maeneo mengi.

Pia ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la kazi duniani ILO inakadiria kwamba kati ya mwaka 2017 na 2019 idadi ya wahamiaji wa kimataifa imeongezeka kutoka milioni 164 hadi milioni 169, sanjari na kuongeza idadi ya wafanyakazi wahamiaji. 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
13'54"