Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

18 JUNI 2021

18 JUNI 2021

Pakua

Katika jarida la mada kwa kina la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea

-Mamilioni ya wakimbizi kuendelea kukabiliwa na njaa endapo msaada wa fedha za msaada hautopatikana limeonya leo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP

-Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR imesema inatiwa wasiwasi miubwa na kuendelea kwa mashambulizi dhidi ya raia na miundombinu yao kwenye jimbo la Marib nchini Yemen, mashambulizi yanayofanywa na kundi la Houthi

-Katika kuelekea siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwenye maeneo yenye mizozo hapo Kesho , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema waathiriwa na mahitaji yao lazima wazingatie wakati juhudi zinaendelea kukomesha jinamizi hilo.

-Mada yetu kwa kina leo inatupeleka Dodoma Tanzania ambako shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO linatoa pembejeo kwa wakulima kuhakikisha kilimo endelevu cha mbogamboga na matunda

-Na katika kujifunza kiswahili leo tuko Uganda kwa Aida Mutenye kupata ufafanuzi wa methali "werevu mwingu huondoa maarifa".

 

Audio Credit
UN News/Assumpta Massoi
Audio Duration
13'3"