Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

June 24, 2021

June 24, 2021

Pakua

Katika Jarida hii leo utasikia Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP, David Beasley, ameiomba dunia kutoipa kisogo Masdagascar ambako maelfu ya watu wanakabiliwa na njaa kali na badala yake kujitoa na kuchukua hatua haraka baada ya kushuhudia mgogoro mkubwa usioonekana wa njaa unaoendelea Kusini mwa nchi hiyo  na kuathiri jamii nzima. 

Pia utasikia kuhusu wasiwasi wa wazazi nchini Palestina juu ya maisha ya baadae ya watoto wao ikiwa nchi yae itaendelea na machafuko. 

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Filippo Grandi amehitimisha ziara yake ya wiki moja ya kutembelea nchi zilizoko Amerika ya Kusini na kuzishukuru nchi hizo kwa kazi kubwa ya kuhifadhi wakimbizi.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'11"