Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

31 AGOSTI 2020

31 AGOSTI 2020

Pakua

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, leo limechapisha utafiti wake wa kwanza wa athari za janga la corona au coronavirus">COVID-19 kwa mifumo ya afya duniani, hali ikoje? Waathirika wa mafuriko makubwa yanayokumba maeneo mbalimbali ya Mashariki mwa Afrika na kusababisha athari  ikiwemo watu kupoteza kila kitu, hususan  nchini Kenya wamelishukuru shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kuwasaidia. Nchini Uganda, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, kwa kushirikiana na serikali, limechukua hatua kuhakikisha kuwa huduma za msingi za kiafya za kuokoa maisha ikiwemo dawa za kupunguza makali ya UKIMWI zinapatikana hata wakati huu wa vizuizi vya ugonjwa wa virusi vya Corona au coronavirus">COVID-19.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'12"