Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

19 Agosti 2020

19 Agosti 2020

Pakua

Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Flora Nducha

-Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibindamu na masula ya dharura OCHA yatoa shukrani zake kwa wahudumu wa kibinadamu kokote waliko katika kuokoa maisha.

- Ikiwa leo ni siku ya huduma za kibinadamu duniani Umoja wa Mataifa umesema unawaenzi wahudumu hao ambao wanakabiliana na changamoto lukuki katika kuokoa na kuboresha maisha ya mamilioni ya watu.

- Miongoni mwa mashujaa watano halisi wa kibinadamu ambao wanatambuliwa hii leo ni Umra Omar, muasisi na mkurugenzi wa shirika la kiraia la Safari Doctors ambalo linatoa huduma za afya ya binadamu na wanyama kwenye kaunti ya  Lamu nchini Kenya.   

- Na kwenye makala leo tunaenda nchini Uganda kumsikia mwanamuziki aliyegeukia kazi ya ufundi seremala baada ya COVID-19 kuvuruga mipango yake ya awali.

-Na leo mashinani  tutakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC , ambako tunakutana na manusura wa Ebola aliyejitolea kumkinga mtoto aliyehatarini kuambukizwa Ebola, Karibu!

 

 

 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
13'27"