Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

25 Agosti 2020

25 Agosti 2020

Pakua

Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Flora Nducha

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres  amesema COVID 19 imeathiri utalii na hivyo kuharibu ajira, uchumi na urithi wa asili

-  Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP yasaka dola milioni 235 kusambaza misaada ya chakula Lebanon kwa miezi 6 ijayo

- Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema mazungumzo na watoto kuhusu tatizo la ubaguzi na ubaguzi wa rangi si suala rahisi lakini ni ya lazima na ni jukumu la wazazi na walezi

-Na kwenye makala leo tutaelekea Uganda kuangazia ushiriki wa wanawake kwenye kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea uchaguzi mkuu mwakani.

-Na kwenye mashinani leo tutakwenda nchini Vietnam  ambako shirika la kazi la Umoja wa Mataifa, ILO limeleta nuru kwa familia zilizoathiriwa na janga la COVID-19, Karibu! 


 

 

 

 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
13'28"