Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

20 Agosti 2020

20 Agosti 2020

Pakua
Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Flora Nducha
- Mashirika ya Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO na la kuhudumia watotoUNICEF zataka shule zifunguliwe kwa njia salama Afrika 
- Nzige vamizi wa jangwani wakiendelea kuharibu mazao kwenye kaunti ya Turkana nchini Kenya, shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO linaendelea na kampeni kubwa ili kupunguza tatizo la ukosefu wa chakula.
-Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake na wadau, wameendelea kutoa misaada kwa waathirika wa mlipuko uliotokea Agosti 4 katika mji mkuu wa Lebanon Beirut. Takribani walinda amani 100, wanajeshi na raia, wamejitolea kuchangia damu kwani bado uhitaji ni mkubwa.
-Na kwenye makala leo tutakuwa Dar es Salaam Tanzania kusikia harakati za mpiga picha ambaye amenuia kuondoa pengo la uchache wa wanawake katika tasnia ya upigaji picha. 

-Na leo mashinani  tutakwenda nchini Uganda  kuangazia jinsi UNICEF na washirika wake wanashughulikia tatizo la utapiamlo  nchini humo Karibu!

 

 

 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
13'12"