Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 Agosti 2020

21 Agosti 2020

Pakua
Jaridani la Umoja wa Mataifa hii leo na Flora Nducha
- Leo ni siku ya kukumbuka na kuenzi waathiriwa na manusura waugaidi, ikiwa ni maadhimisho ya tatu tangu Baraza Kuu la Umoja
wa Mataifa lipitishe azimio la kutambua siku hii mwaka 2018
- Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filippo Grandi amewatembelea wakimbizi ambao ni waathirika wa mlipuko wa wiki iliyopita mjini Beirut nchini Lebanon kuwapa pole.
- Na, idadi ya wagonjwa wa Ebola kwenye jimbo la Equateur nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC imefikia 100, ikiwa ni ongezeko maradufu katika kipindi cha wiki 5.
-Na katika mada kwa kina tunakwenda Kenya kukutana na manusura wa shambulio la kigaidi ambaye baada ya kunusurika kwenye
shambulio la kigaidi na kushuhudia kile ambacho yeye na manusura au waathiriwa wengine wanapitia baada ya kukumbwa
na mkasa.

-Na katika kujifunza kiswahili leo tunaangazia maana ya methali"Hakuna mchele ukosao ndume na hakuna masika yasiyo na mbu"Karibu!

 

 

 

 

 

 
Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
10'24"