Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

28 AGOSTI 2020

28 AGOSTI 2020

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema janga la corona au COVID-19 limeanika wazi mifumo tete na pengo la usawa vitu ambavyo vinatishia msingi wa maendeleo endelevu, SDGs.  Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, limeendelea na juhudi zake za kusaidia kupambana na utapiamlo kwa watoto nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ingawa coronavirus">COVID-19 inatishia shughuli hizo znazolenga kuwaokoa watoto wapatao milioni 3.4. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet ameeleza wasiwasi wake juu ya vitisho vya hivi karibuni vya mauaji dhidi ya mtetezi wa haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemorkasia ya Congo, DRC na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Dkt. Dennis Mukwege.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'46"