Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

© UNICEF/Eyad El Baba

Fahamu nini kinaweza kufuatia pindi maazimio yanagonga mwamba Baraza la Usalama la UN

Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiendelea kati ya Israeli na kundi la wanamgambo wa kipalestina, Hamas, hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye jukumu la kusimamia amani na usalama liko njiapanda baada ya rasimu mbili za maazimio kwa ajili ya kuchukua hatua kwenye mzozo huo kugonga mwamba! Marekani ikitumia kura turufu. Sasa nini kinafuatia? Rasimu mpya au kikao cha dharura cha Baraza Kuu? 

Bila shaka Assumpta! Ikumbukwe kuwa mzozo wa sasa huko Mashariki ya Kati alianza tarehe 7 mwezi huu wa Oktoba kwa Hamas kurusha makombora Israel.

Sauti
3'51"
TANZBATT 10

Tunashukuru TANZBATT10 kwa vifaa vya shule lakini pia watusaidie majengo

Hii leo katika makala ninakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, kikosi cha 10, TANZBATT 10 kinachohudumu kwenye ujumbe wa UN wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, hususan kile cha kujibu mashambulizi, FIB wamefika shule ya msingi Ushindi mjini Beni, jimboni Kivu Kaskazini na kutoa msaada wa vifaa vya shule wakilenga kufanikisha lengo namba 4 la malengo  ya maendeleo endelevu. SDGs hukusan kipengele kinachohusu ujumuishi.

Sauti
3'28"
UN Ukraine

Umoja wa Mataifa unaendelea kuwapatia msaada wananchi waliosalia nchini Ukraine

Uvamizi wa Urusi  nchini Ukraine umefurusha makwao mamilioni ya watu kwenda kusaka hifadhi maeneo ya mikoani na hata nchi jirani. Katika Mkoa wa Donetsk asilimia 90 ya wananchi walikimbia tu vita ilipoanza, na zaidi ya wananchi 1,000 walioamua kusalia hawana huduma za maji, umeme na gesi na Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kila juhudi kuhakikisha wanapata huduma hizo muhimu.

Wakazi wa Chasiv Yar mkoani Donetsk tangu kuibuka kwa vita kati ya Ukraine na Urusi wamekuwa wakiishi katika hali ya taabu na kujificha katika mahandaki chini ya nyumba zao.

Sauti
2'26"
© UNICEF/Eyad El Baba

Guterres: Mapigano lazima yasite mara moja Gaza kwa sababu za kibinadamu

Hali Mashariki ya Kati inaendelea kuwa mbayá hasa baada ya shambulio dhidi ya Hospitali ya Al-Ahli na kukatili Maisha ya zaidi ya watu 500. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelazimika kukatisha ziara yake nchini China na kuelekea Cairo Misri lakini kabla ya kuondoka ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano Mashariki ya kwa ajili ya masuala ya kibinadamu. Naye mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths ameshawasili Cairo Misri katika juhudi za kuhakikisha misaada inaruhusiwa kuingia Gaza. 

Sauti
3'15"
WHO

Matarajio ya OCHA ni misaada ya kibinadamu kuruhusiwa kuingia Gaza

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Martin Griffiths, ameeleza wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa mzozo wa kibinadamu huko Gaza, Mashariki ya Kati, kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya Israel na wanamgambo wa kipalestina, Hamas, halikadhalika hatma ya mateka wa Israel, huku pia akieleza matarajio yake ya kupokea habari njema za misaada kuruhusiwa kuingia Gaza. 

Sauti
3'7"
© FAO/Seyllou Diallo

FAO inasisitiza kwamba maji ni uhai, maji ni chakula tusimwache yeyote nyuma katika hili

Leo ni siku ya chakula duniani na maadhimisho ya mwaka huu kwa mujibu wa shirika na chakula na kilimo FAO yanasherehekea moja ya rasilimali muhimu zaidi kwa maisha ya binadamu ambayo ni maji, kwani yanachukua asilimia 50 ya uso wa dunia, yanazalisha chakula na kuwezesha watu kuishi. 

Maudhui ya siku ya mwaka huu ni “Maji ni uhai, maji ni chakula, usimwache yeyote nyuma”.

Sauti
2'51"
WHO/Occupied Palestinian Territory

Raia katika ukanda wa Gaza hawana pa kukimbilia, milioni 1 waambiwa waondoke ndani ya saa 24: UN

Leo ni siku nyingine ambapo hali imeendelea kuwa tete na mbayá zaidi kwenye Ukanda wa Gaza, kwani Israel imetangaza watu wote wanaoishi katika eneo la Kaskazini mwa Wadi Gaza kuondoka na kwenda Kusini mwa Gaza ndani ya saa 24 na hivyo kuwaacha njiapanda maelfu kwa maelfu ya watu wanaoishi eneo hilo yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa hii leo ambayo yanahaha kuwasaidia na kuwanusuru watu hao. 

Sauti
2'49"
UNOCHA/Martin San Diego

Tushirikishe watoto katika kujiandaa na athari za majanga unamanufaa - UNICEF

Ufilipino ni mojawapo ya nchi zinazokabiliwa zaidi na hatari za majanga duniani, jimboni Samar Kaskazini, hatari kwa watoto ni kubwa zaidi ndio maana Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linafanya kazi na serikali za mtaa ili kuwashirikisha watoto na vijana katika hatua za kujiandaa na hatari pamoja na kupunguza athari za majanga kama anavyotujuza Leah Mushi katika taarifa hii aliyotuandalia.

Sauti
3'26"
© IOM

Mashirika ya kibinadamu nayo yanahitaji msaada ili kusaidia wakimbizi wa Armenia

Mashirika ya kibinadamu nayo yanahitaji msaada ili kusaidia wakimbizi wa Armenia 

Ili kuhakikisha mahitaji ya muda mfupi, kati na ya muda mrefu yanatimizwa, mashirika ya kibinadamu yanaendelea kuhaha kutafuta ufadhili wa haraka ili kuongeza msaada kwa zaidi ya wakimbizi 100,000 nchini Armenia waliokimbia eneo la Karabhak kufuatia kuongezeka kwa uhasama mwezi Septemba. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Anold Kayanda)

Sauti
1'46"