Sera za MPOWER zaepusha watu kuvutishwa sigara bila ridhaa yao- WHO
Miaka 15 baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO kuanzisha sera ya kulinda umma kutoathirika na uvutaji wa sigara unaofanywa na mtu mwingine, zaidi ya watu bilioni 5.6 wamenufaika na sera hiyo ulimwenguni kote, imesema ripoti mpya ya shirika hilo iliyotolewa leo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Assumpta Massoi.