Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

© Ziad Taleb

Wanawake na wasichana wajawazito walioko Gaza wasimulia kinachowakumba

Wakati mzozo katika Ukanda wa Gaza ukizidi kuongezeka huku wananchi wakikabiliwa na changamoto nyingine lukuki ikiwemo uhaba wa chakula, maji, mafuta na vifaa vya matibabu vya kuokoa maisha, Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu na Afya ya Uzazi UNFPA limesema mfumo wa afya nao uko ukingoni kuanguka. Shirika hilo limezungumza na wanawake wajawazito walioko Gaza kuhusu hali mbaya wanayokabiliana nayo. Thelma mwadzaya anatujuza walichosema wanawake hao. 

Sauti
3'9"
© WFP/Eulalia Berlanga

Sikuwa nataka kurejea nchini mwangu Sudan Kusini - Mkimbizi kutoka Sudan

Wakati maelfu ya wananchi wakikimbia machafuko nchini Sudan mashirika ya Umoja wa Mataifa nayo yana haha huku na kule kuhakikisha wanatoa usaidizi kwa wakimbizi hao. 

Tangu kuibuka kwa mzozo nchini Sudan miezi sita iliyopita, takriban watu milioni 6 wamelazimika kuyakimbia makazi yao wakisaka hifadhi katika nchi jirani zikiwemo Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Misri, Ethiopia na Sudan Kusini. 

Audio Duration
2'29"
MONUSCO

Wanawake kwenye INDIBAT-1 waleta matumaini kwa wanawake Nchini DRC

Mwezi huu wa Oktoba ikiwa ni miaka 23 tangu kupitishwa kwa azimio namba 1325 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake katika harakati za amani na usalama ninakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikia jinsi ujumuishaji wa wanawake walinda amani kwenye kikosi cha India kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo (MONUSCO) kumeleta matumaini kwa wanawake. 

Sauti
2'41"
© UNICEF/Eyad El Baba

Fahamu nini kinaweza kufuatia pindi maazimio yanagonga mwamba Baraza la Usalama la UN

Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiendelea kati ya Israeli na kundi la wanamgambo wa kipalestina, Hamas, hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye jukumu la kusimamia amani na usalama liko njiapanda baada ya rasimu mbili za maazimio kwa ajili ya kuchukua hatua kwenye mzozo huo kugonga mwamba! Marekani ikitumia kura turufu. Sasa nini kinafuatia? Rasimu mpya au kikao cha dharura cha Baraza Kuu? 

Bila shaka Assumpta! Ikumbukwe kuwa mzozo wa sasa huko Mashariki ya Kati alianza tarehe 7 mwezi huu wa Oktoba kwa Hamas kurusha makombora Israel.

Sauti
3'51"
TANZBATT 10

Tunashukuru TANZBATT10 kwa vifaa vya shule lakini pia watusaidie majengo

Hii leo katika makala ninakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, kikosi cha 10, TANZBATT 10 kinachohudumu kwenye ujumbe wa UN wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, hususan kile cha kujibu mashambulizi, FIB wamefika shule ya msingi Ushindi mjini Beni, jimboni Kivu Kaskazini na kutoa msaada wa vifaa vya shule wakilenga kufanikisha lengo namba 4 la malengo  ya maendeleo endelevu. SDGs hukusan kipengele kinachohusu ujumuishi.

Sauti
3'28"