Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres: Mapigano lazima yasite mara moja Gaza kwa sababu za kibinadamu

Guterres: Mapigano lazima yasite mara moja Gaza kwa sababu za kibinadamu

Pakua

Hali Mashariki ya Kati inaendelea kuwa mbayá hasa baada ya shambulio dhidi ya Hospitali ya Al-Ahli na kukatili Maisha ya zaidi ya watu 500. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelazimika kukatisha ziara yake nchini China na kuelekea Cairo Misri lakini kabla ya kuondoka ametoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mapigano Mashariki ya kwa ajili ya masuala ya kibinadamu. Naye mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa Martin Griffiths ameshawasili Cairo Misri katika juhudi za kuhakikisha misaada inaruhusiwa kuingia Gaza. 

Akizungumza mjini Beijing China, kabla ya kuondoka kuelekea Cairo Misri hii leo Bwana Guterres hakutafuna maneno, amesema kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anawajibika kutoa kauli hii ili kupunguza madhila makubwa yanayowaghubika watu katika mzozo wa Masharikiya Kati Mashariki ya Kati ni "mateso makubwa ya kibinadamu" 

 Hivyo amesema “Natoa wito wa usitishaji mapigano haraka kwa sababu za kibinadamu ili kutoa wakati na fursa ya kutosha kusaidia kutimiza maombi yangu mawili na kupunguza mateso makubwa kwa binadamu tunayoshuhudia. Maisha ya watu wengi na hatma ya ukanda mzima viko njiapanda.”

Guterres ameonya kwamba eneo mzima liko katika hatari ya janga kubwa akisisitiza umuhimu wa kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.

Wakati huohuo mratibu wa masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura Martin Griffiths ameshawasili Cairo Misri kwa ajili ya kuhakikisha misaada hiyo ya kibinadamu ambayo iko tayari mpakani mwa Gaza inaruhusiwa kuingia ili kuokoa maisha ya watu wengi. Kupitia ukurasa wake wa X amesema “ Kutoa misaada kwa watu wa Gaza popote walipo ni suala la uhai au kifo. Kufanya hivyo kwa njia endelevu, isiyozuiliwa, na inayotabirika ni sharti la kibinadamu.”

Naye Phillippe Lazzarini kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA amewaomba mawaziri wa mambo ya nje wa jumuiya ya ushirikiano wa nchi za Kiislamu OIC "kuunga mkono kwa dhati na bila masharti juhudi za kibinadamu za kuwalinda raia huko Gaza"  akisema kwani hadi sasa “Hakuna shehena hata moja ya msaada imeruhusiwa kuingia Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa mzozo huu kutokana na hali iliyowekwa na Israel  ya kuzingizwa. Watu wanalazimika kunywa maji ambayo hayafai kwa matumizi, kwani maji safi ya kunywa hayapatikani. Akiba ya chakula, vifaa vya usafi na dawa vinapungua kwa kasi. Tuko ukingoni mwa janga kubwa la afya na usafi wa mazingira”.

Hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa Baraza la Usalama limekutana kujadili mgogoro huo na huko Israel Rais wa Marekani Joe Biden amewasili na kukutana na waziri mkuu Benjamin Netanyahu ambapo ameahidi msaada wa Marekani kwa Israel na kusema ameshtushwa na kughadhibishwa na mlipuko wa jana katika hospital mjini Gaza. 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
3'15"
Photo Credit
© UNICEF/Eyad El Baba