Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunashukuru TANZBATT10 kwa vifaa vya shule lakini pia watusaidie majengo

Tunashukuru TANZBATT10 kwa vifaa vya shule lakini pia watusaidie majengo

Pakua

Hii leo katika makala ninakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, kikosi cha 10, TANZBATT 10 kinachohudumu kwenye ujumbe wa UN wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO, hususan kile cha kujibu mashambulizi, FIB wamefika shule ya msingi Ushindi mjini Beni, jimboni Kivu Kaskazini na kutoa msaada wa vifaa vya shule wakilenga kufanikisha lengo namba 4 la malengo  ya maendeleo endelevu. SDGs hukusan kipengele kinachohusu ujumuishi. Afisa Habari wa kikosi hicho  Luteni Abubakari Muna ameandaa makala hii kutoka na ziara hiyo, ikianza na Meja Neema Neligwa mwakilishi wa Kamanda kikosi cha TANZBATT 10, Luteni Kanali John Peter Kalabaka akifafanua walengwa kwa msaada huo. 

Audio Credit
Assumpta Masoi/Luteni Abubakari Muna
Sauti
3'28"
Photo Credit
TANZBATT 10