Mashirika yashirikiana kusambaza chakula Sudan
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Sudan limesema linaendelea kufanya kazi kwa karibu na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP ili kuona ni kwa vipi chakula kilichomo nchini humo kinawza kusambazwa kwa wahitaji na wakati huo huo misaada mingine inaweza kutolewa kwa ushirikiano na wadau wengine wakati huu ambapo uhasama unashamiri na kuathiri raia wakiwemo wakimbizi, wakimbizi wa ndani na raia nchini kote.