Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

17 JANUARI 2020

Katika Jarida la makala kwa kina Ijumaa ya leo Grace Kaneiya anakuletea

- Ripoti mpya ya shirika la afya duniani WHO, leo limeonya kwamba upungufu wa dawa mpya za viuavijasumu au antibiotics unatishia unatishia juhudi za kukabiliana na usugu wa dawa hizo na hivyo kuweka njiapanda maisha ya mamilioni ya watu

-Kamishina mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa OHCHR, Michelle Bachelet aleo amelaani vikali kuendelea kwa mauaji na ukatili mwingine Kaskazini Magharibi mwa Syria hasa jimbo la Idlib licha ya kutangazwa usitishaji mapigano wiki iliyopita

Sauti
9'57"
UNICEF/Julio Dengucho

UNESCO imesema kimbunga Idai kilitoa picha halisi ya hali ya watu wanoishi na ulemavu Zimbabwe

Wakati kimbunga Idai kilipiga nchi mbali mbali ikiwemo Zimbabwe kuna baadhi ya watu katika jamii hususan wanaoishi na ulemavu walikuwa hatarini na ilikuwa ni vigumu kwao kufikiwa na msaada, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO lililoandaa video mahsusi kwa ajili ya kutoa elimu kuhusu suala hilo.

Sauti
2'50"

15 JANUARI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo Grace Kaneiya anakuletea

-Ripoti mpya iliyotolea na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA inasema hatua za haraka zinahitajika ili kunusuru maisha ya maelfu ya wanawake wajawaziti na watoto wanaozaliwa Darfur Magharibi baada ya kutawanywa na machafuko ya kikabila

-Msimu wa baridi umeelezwa kuongeza madhila zaidi kwa maelfu ya watu Idlib Syria hususan watoto kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF

Sauti
11'23"